Feature Tanzania
RAIS DKT. MAGUFULI AZINDUA JENGO LA KITEGAUCHUMI LA MFUKO WA PENSHENI PPF JIJINI ARUSHA
![]() |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akikata utepe kuzindua rasmi, Jengo la Kitegauchumi la Mfuko wa Pensheni (PPF) lililopo Mtaa wa Korido Jijini Arusha leo Mei 9, 2016. Wa pili (kushoto) ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu na Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Jenister Mhagama, (kushoto) ni Meya wa jiji la Arusha, Calist Lazaro (wa kwanza kutoka kulia) ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya PPF, Ramadhan Kijjah, Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango. |
![]() |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akimpongeza Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio, baada ya kuweka Jiwe la Msingi la uzinduai wa Jengo la Kitegauchumi la Mfuko huo lililopo Mtaa wa Korido Jijini Arusha leo Mei 9, 2016. |


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli,
akihutubia wakazi wa arusha na wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF wakati
alipozindua rasmi, Jengo la Kitegauchumi la Mfuko huo (PPF) lililopo
Mtaa wa Korido Jijini Arusha leo Mei 9, 2016.

Sehemu ya wadau kutoka NSSF waliohudhuria uzinduzi huo wa wenzao wa PPF.

Sehemu ya wadau wakimsikiliza Mhe. Rais Dkt. Magufuli.....

Baadhi ya wafanyakazi wa PPF Kanda yas Arusha wakimsikiliza Mhe Rais wakati akihutubia.

Wananchi wakimshangilia Mhe Rais wakati akihutubia.....

Baadhi ya Wakurugenzi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF wakimsikiliza Mhe Rais wakati akihutubia.

Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Pensheni PPF na
Wakurugenzi wa Mfuko wa huo wakimsikiliza Mhe Rais wakati akihutubia.

Baadhi ya viongozi na wadau wa Mfuko huo na Meya wa Jiji la Arusha Calist Lazaro (kushoto) wakimsikiliza Mhe Rais.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli,
akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi PPF, Ramadhan Kijjah,
wakati alipowasili kwenye Viwanja vya Jengo la Kitegauchumi la Mfuko wa
Pensheni PPF lililopo Mtaa wa Korido jijini Arusha kwa ajili ya uzinduzi
wa jengo hilo leo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli,
akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio, wakati alipowasili
kwenye Viwanja vya Jengo la Kitegauchumi la Mfuko wa Pensheni PPF
lililopo Mtaa wa Korido jijini Arusha kwa ajili ya uzinduzi wa jengo
hilo leo.

Wakifurahia baada ya uzinduzi huo....

Picha ya pamoja baada ya uzinduzi huo.
Picha ya pamoja baada ya uzinduzi huo.

Viongozi wakiwa meza kuu wakiimba wimbo wa Taifa
Meya Kinondoni atumbua majipu, yupo Mwanasheria Mkuu Mahenge
![]() |
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Mh. Boniface Jacob |
Akisoma taarifa na nyaraka mbalimbali mbele ya wanahabari, Mh. Boniface Jacob alieleza kuwa: Kikao cha Kamati ya fedha na Uongozi cha tarehe 29/04/2016, kiliagiza kuwa yaorodheshwe mashauri yote ambayo hayakusimamiwa vizuri na Mwanasheria wa Manispaa Bwana Burton Mahenge, na hivyo kuisababishia Manispaa kupata hasara, kupoteza mali, na kuchelewa kupata manufaa katika mali zake.
“Kufuatia makosa yaliyogundulika katika mashauri hayo, baraza la
Madiwani la terehe 04/05/2016, limeamua
kuwasimamisha kazi Mwanasheria Mkuu wa Manispaa Bw. Burton Mahenge, na
Mthamini wa Manispaa Bw. Einhard Chidaga”.
Mh. Boniface Jacob aliyataja Makosa yaliyogundulika katika Mashauri hayo ni kama yafuatayo:-
Mh. Boniface Jacob aliyataja Makosa yaliyogundulika katika Mashauri hayo ni kama yafuatayo:-
Mradi wa uwekezaji wa Oysterbay Villa.
Mkataba huo, ulifanyiwa marekebisho
mbalimbali bila idhini ya Halmashauri na hali hiyo kumpatia sauti zaidi
Mwekezaji na kuamua analotaka. Manispaa ilipaswa kupata shilingi milioni
900 kwa mwaka katika uwekezaji huo,lakini kutokana na Mgogoro wa
kimkataba mapato hayo hayajawahi kulipwa hivyo kupoteza shilingi billion
4.5 mpaka sasa. Mradi ulikamilika tangu 2011 katika viwanja vyote
viwili kiwanja Na.277 na 322 ambapo uwekezaji katika kiwanja namba 277
una nyumba (Apartments) 44 na katika kiwanja Na.322 nyumba 68 (Mwekezaji
nyumba 29 KMC Nyumba 17)
2 .Mgogoro wa wapangaji wa Nyumba za Magomeni Kota.Manispaa iliandaa mpango wa kuendeleza eneo la Magomeni Kota , hivyo kuwaondoa wapangaji hao na kubomoa nyumba hizo kongwe. Wapangaji walifungua shauri la kupinga kuondolewa katika nyumba, na kutoa madai ya kujengewa
nyumba,ama kulipwa fedha za fidia
kutokana na usimamizi hafifu wa shauri hili Mahakama imeruhusu iliamuru
Manispaa kukaana kumalizana na wapangaji nje ya mahakama. Halmashauri
ikatengeneza mkataba wa kuwalipa wapangaji kiasi cha shilingi
1,080,000/= kwa kila mpangaji kama kodi ya Mwaka na kumpatia kila
mpangaji kiwanja.Hivyo Manispaa inatakiwa kulipa shilingi
3,271,520,000/= kugharamia fidia hiyo,kwa mchanganuo wa
Tshs.695,520,000/= pango la mwaka na Tsh2,576,000,000/=fidia ya viwanja
644.
3.Uwekezaji Eneo la Coco Beach Oysterbay.
Manispaa iliingia Mkataba wa Q-Consult Limited. Kampuni hiyo ilishindwa kutekeleza mradi kwa wakati na Manispaa ikavunja Mkataba huo. Q-consult Limited ilifungua shauri ambalo halikusimamiwa vizuri na kwa sababu ya kutofika kwenye kesi, Manispaa ilipoteza kesi hiyo. Halmashauri iliagiza kukata kwa rufaa lakini hakukuwa na hatua zozote zilizochukuliwa, na hivyo Manispaa inaweza kupoteza haki yake. Iliagizwa na serikali mwanasheria mkuu baada ya tamko la Rais Mhe. John Pombe Magufuli kutangaza nia ya kutoachia eneo hilo mpaka sasa mwanasheria alikuwa hajakata rufaa.
4.Mradi wa ujenzi wa maduka Makumbusho (Eastern Capital LTD)
Katika shauri hili mabadiliko ya mradi yalifanyika bila idhini ya Halmashauri kwa kubadili michoro na kuongeza maeneo mengine katika mradi kama vile kituo cha Mabasi , Matangazo na choo. viwango vya mgawanyo wa mapato ya Manispaa katika maeneo yaalioongezewa ni kidogo ukilinganisha na uhalisia.
Halmashauri haina mkataba na mwekezaji kwa baadhi ya uendeshaji wa majengo ‘above two storey’hazipo kwenye kumbukumbu za Halmashauri.
Mkataba juu ya ujenzi na uendeshaji wa stendi hauna manufaa kwa Halmashauri ,KMC inapata 1%ya makusanyo kwa mwaka sawa na mil.4 tu kwa mwezi wakati kabla ya uwekezaji ,local standy Halmashauri ilikuwa ikipata 12mil. kwa mwezi.
5.Kubomolewa Kwa Ofisi ya Kata ya Msasani.
Mwanachi aliyejulikana kwa jina la Chacha aliingilia eneo la Ofisi ya Kata Msasani na baadae kuishitaki Manispaa.Usimamizi dhaifu wa shauri hilo ulisababisha mahakama kutoa amri ya kubomoa ofisi ya Kata, Manispaa imekata rufaa na sasa ni muda mrefu shauri halisikilizwi na hakuna ufuatiliaji unaoendelea. Hata hivyo bwana Chacha kwa makusudi aliamua kuuza kiwanja hiki, kwa Lake Oil Co. Limited wakati shauri halijaisha. Manispaa imekosa manufaa mengi kwa kuchelewa kukamilika kwa shauri hilo.Tangu upandewa pili ulikataa jaji.Tuna zaidi ya mwaka hatuja pangiwa jaji mwingine na hatujafuatilia kama Halmashauri.
6.Ujenzi wa Nyumba za Makazi. (Apartments ) Hill Road Oysterbay
Mradi unafanyika kwa ubia na Mwekezaji Texas Enterprise company LTD, Mkataba uliingiwa mwaka 2009, na Mradi umesimama kwa Muda Mrefu sasa.
Pamefanyika mabadiliko katika Mkataba na Mkataba umefanyiwa marekebisho bila idhini ya Halmashauri. Manispaa inakosa manufaa ya Mali yake kwa sababu ya kuchelewa kwa Mradi. Lakini pia uendeshaji mpya wa sasa hauna makubaliano wa Financial proposal na Investment capital.
Ujenzi wa nyumba za Makazi(Apartments).Kiwanja Na. 314 Toure Drive.
Mradi huu unatekelezwa kwa ubia na Kampuni ya Lake Oil Limited. Mkataba uliingiwa 2019. Mabadiliko yamefanyika katika Mkataba bila Idhini ya Halmashauri na kusababisha Mradi kuchelewa kukamilika. Manispaa inakosa Manufaa ya Mali yake kwa kuchelewa kukamilika mradi huu.
Aidha, Mh. Boniface Jacob amesema kuwa, itakuwa ni jambo la aibu kwa Manispaa kushindwa kuchukua hatua suala la mradi wa Coco Beach, licha ya Rais Dk. John Pombe Magufuli kutaka eneo hilo libaki kuwa mali ya wananchi na si kumuachia mwekezaji kuweka miradi yake.
Hata hivyo Mwanasheria huyo wa Manispaa hakuweza kuchukua hatua yoyote hadi sasa hivyo kuonekana bado mchezo unachezwa hivyo maamuzi ya kusimamishwa ambapo pia licha ya kusimamishwa, Meya huyo amebainisha kuwa, atachukuliwa hatua za kinidhamu na kisheria kwa mamlaka husika za Kiserikali.
Subscribe to:
Posts (Atom)